Home Soka Guede Afungua Akaunti ya Mabao Yanga sc

Guede Afungua Akaunti ya Mabao Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga sc Joseph Guede ameanza rasmi kazi ya kutupia nyavuni baada ya kufanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 ilioupata Yanga sc dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumanne jioni.

Guede alifunga mabao hayo dakika za 13 na 45 akipokea pasi nzuri kutoka kwa Augustine Okrah ambapo alifanikiwa kufunga mabao hayo kwa kichwa vikalina kuzua shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao hawakua wengi uwanjani katika uwanja wa Chamazi.

Kufunga huko kumempunguzia presha mshambuliaji huyo ambaye hakua amefunga katika michezo mitano ya ligi kuu tangu asajiliwe na klabu hiyo wakati wa dirisha dogo msimu huu na kuzua minong’ono kwa mashabiki hasa wa upinzani wakiwacheka kuwa wamepigwa.

banner

Yanga sc siku ya Jumamosi itakua na mchezo dhidi ya Cr Belouzdad  wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo inawezekana pia staa huyo akaanza kama mshambuliaji kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na kuanzisha mashambulizi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited