Home Soka Hata Mimi Sielewi-Ajibu

Hata Mimi Sielewi-Ajibu

by Sports Leo
0 comments

Staa wa klabu ya Simba sc Ibrahimu Ajibu ameshangazwa na kauli za kocha mkuu wa timu hiyo Sven Vandebroek kuwa hajitumi na ndio maana hapati nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Sven alisema kuwa hawapangi baadhi ya wachezaji kama Ajibu na Kichuya kutokana na kuwa na viwango vya kawaida  pindi wanapopata nafasi tofauti na mastaa wengine wa timu hiyo kama Cletous Chama,Deo Kanda,Luis Miquissone.

Akijibu tuhuma hizo staa huyo alisema hata yeye ameshangazwa a kauli hizo kwa kuwa amekua akijituma sana mazoezini na kwenye mechi.

banner

“Nafahamu kikosi chetu kina wachezaji wazuri katika kila nafasi hivyo ushindani kuongezeka katika kila idara,kwa jinsi navyojituma mazoezini huwa nahisi kuumwa pindi ninapokosa nafasi ya kucheza kwenye ligi na mashindano mengine”Alisema staa huyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited