Home Soka Kipa Stars Abaki Kidogo Tu Yanga

Kipa Stars Abaki Kidogo Tu Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kamati ya usajili ya Yanga ambayo imetua nchini Misri kwa ajili ya kazi maalumu ya kuhakikisha inamalizana na mastaa ambao ilifanya nao mazungumzo kuhusu kutua klabuni hapo na baada ya kumalizana na beki Ally Mtoni Sonso na kipa mkenya wa Bandari Fc Farouk Shikalo na sasa kamati hiyo imetua kwa kipa Metacha Mnata.

Kipa huyo amabye yupo kwenye kambi ya taifa stars tayari alishafanya mazungumzo na klabu hiyo yenye fedha za michango kutoka kwa wanachama na sasa imekuja kukamilisha mazungumzo hayo na kusaini mkataba ili kuwahi kutuma jina la kipa huyo shirikisho la soka barani afrika (Caf).

Yanga tayari imewanasa mastaa kadhaa wa ndani na nje ya nchi na sasa inataka kujaza nafasi ya golikipa baada ya kumalizana na Shikalo ili iwe na makipa watatu akiwemo kinda Ramadhani Kabwili na Mkongomani Klaus Kindoki anaweza kutupiwa virago klabuni baada ya kushindwa kuushawishi uongozi wa klabu hiyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited