Kocha wa zamani wa klabu ya Simba sc Masoud Djuma amewapa tano klabu ya Yanga baada ya kusikia wanaisaka saini ya kiungo wa Rwanda Ally Niyonzima.
Kocha huyo ambaye amewahi kumnoa kiungo huyo wakati akiifundisha klabu ya As Kigali mwaka 2018 alisema kama Yanga watakamilisha dili hilo watakua wamelamba dume kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi tatu uwanjani.
Kwa mujibu wa kocha huyo mwenye mizuka awapo uwanjani Niyonzima ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati pamoja na kiungo mkabaji au mshambuliaji.