Home Soka Man Utd Yaichachafya Shelfied

Man Utd Yaichachafya Shelfied

by Sports Leo
0 comments

Athony Martial amefunga Hat trick yake ya kwanza baada ya Takribani miaka saba baada ya kuisadia Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Shelfied United katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Mfaransa huyo alifunga mabao hayo dakika za 7,44 na 74 na kumaliza ukame wa Hat trick kikosini humo ambapo mara ya mwisho mchezaji wa United kufunga mabao matatu ilikua na msimu wa 2012/2013 ambapo Robin Van Persie alifunga dhidi ya Aston Villa na kuipa United taji la 20 la ligi kuu.

Ushindi huo umeifanya Man utd kubakisha pointi mbili kuingia katika nafasi nne za juu katika ligi hiyo inayoendelea leo ambapo Chelsea atamvaa Man city.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited