Home Soka Mlandege Bingwa Mapinduzi Cup

Mlandege Bingwa Mapinduzi Cup

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Mlandege Fc imeibuka mabingwa wa kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuifunga Simba sc kwa bao 1-0 katika mchezo wa michuano hiyo uliofanyika katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Mlandege Fc iliyoanza mchezo huo ikijilinda zaidi huku ikishambulia kwa kushtukiza ikiaacha viungo wa Simba Sc Babacar Sarr na Fabrice Ngoma kumiliki mpira huku wao wakiziba zaidi nafasi za pasi za mwisho kuelekea golini kwao na kuwafanya Simba sc wakose njia za kupenya.

Mlandege walifanya shambulizi la kushtukiza kipindi cha pili na kupata bao zuri lililofungwa na Joseph Akandwanao akitumia juhudi na maarifa binafsi kuwapita mabeki wa Simba sc wakiongozwa na Che Fondoh Malone na Hussein Kazi.

banner

Bao hilo lilidumu mpaka dakika tisini za mchezo huo licha ya juhudi za Mwalimu Abelhack Benchika kufanya mabadiliko ya kikosi ili kupata bao la kusawazisha.

Wachezaji Fabrice Ngoma na Elvis Rupia na Kipa wa Mlandege Fc walipata zawadi ya mfungaji bora,kipa Bora na Mchezaji bora wa michuano hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited