Home Soka Moto wa Balinya Usipime Moro

Moto wa Balinya Usipime Moro

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa Yanga sc Mganda Juma Balinya (JB) ni kama ameuwasha moto huko kambini Morogoro ambako kikosi hicho kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambayo kikosi hicho kitashiriki.

Balinya aliyetoka kuwa mfungaji bora wa ligi ya Uganda ameuwasha moto ambao kuuzima inabidi mabeki wa ligi kuu itabidi wajipange kwani kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi anachokifanya mshambuliaji huo ni kufunga tu hali iliwafurahisha benchi la ufundi na mashabiki wachache wanaojitokeza mazoezini hapo.

Balinya alianza kufunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzanite fc na baadae jana asubuhi alifunga tena katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Moro Kids huku mazoezini ndo akitupia kila siku.

banner

Kwa upande wa Kalengo aliyeanza na moto kama wa Balinya lakini alipata maumivu ya kifundo cha mguu hali iliyomlazimu kukaa nje kupata matibabu ili kuwa fiti huku Sydney Ulikhob yeye amechelewa kuripoti hivyo anahitaji muda kidogo ili kurudi katika utimamu wa mwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited