Home Soka Ngassa Wala Hana Hofu

Ngassa Wala Hana Hofu

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Yanga Mrisho Khalfani Ngassa amesema hana hofu juu ya kusaini mkataba mpya na timu baada ya ule wa awali kufika tamati msimu huu,Kiungo huyo mjanja mjanja amedai hahofii suala la mkataba mpya baada ya viongozi kumhakikishia kumsaini hivi karibuni baada ya kocha Zahera kuwataka kufanya hivyo.

Inaripotiwa kuwa Yanga imemtaka winga huyo mzaliwa wa kanda ya ziwa kusubiri kuitwa kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya japo hajajua ni lini haswa ataitwa licha ya kuwa ana ofa kibao mezani za ndani na nje ya nchi.

“Nina taarifa za uongozi kunihitaji kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya japo sijajua ni lini ila tayari nina ofa za ndani na nje hasa kutoka Zambia” Alisema ngasa.

banner

Kiungo huyo mshambuliaji ni mmoja ya wachezaji wenye mapenzi na Yanga huku akifanikiwa kuitumikia kwa vipindi tofauti tofauti huku pia akiwa ni mmoja ya wachezaji waliozitumikia timu kubwa za nchini Yanga,Azam na Simba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited