Home Soka Saido Aaga Simba sc

Saido Aaga Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Saido Ntibanzokiza ameaga mastaa wenzake klabuni hapo baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu huku kila upande ukiwa hauonyeshi nia hasa ya kufungua mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.

Saido alijiunga na Simba sc dirisha dogo la mwezi januari msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambapo msimu huu tayari mkataba huo ukiwa unaisha juni 30 mwaka huu na mpaka sasa uongozi haujamuita kujadili kuongeza mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo.

Saido ni moja ya mastaa waliofanya vizuri ambapo amefunga mabao 11 katika ligi kuu msimu huu na msimu uliopita aliibuka mfungaji bora akifungana na Fiston Mayele baada ya kila mmoja kufunga mabao 18 ya ligi kuu ya Nbc huku pia akiitwa katika kikosi bora cha msimu wa ligi kuu.

banner

Tayari klabu za APR ya Rwanda na Arta Solar ya Djibout zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo ambapo inatajwa kuwa anaweza kwenda nchini Rwanda ambapo klabu hiyo imeonekana kuwa seriazi na dili hilo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited