Home Soka Samatta Ageuka Lulu

Samatta Ageuka Lulu

by Sports Leo
0 comments

Timu za Newcastle united,Westham united na nyinginezo barani ulaya zimeonyesha nia ya kumsajili staa wa kitanzania Mbwana Samatta baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Samatta anayeichezea Krc Genk ya nchini Ubeligiji amegeuka lulu baada ya kucheza michuano hiyo na kufanikiwa kuwakabili mabeki bora duniani akiwemo Virgil Van Djik na kufanikiwa kufunga goli katika mechi ya marudiano baada ya awali kufunga katika mechi ya kwanza bao lililokataliwa na mwamuzi wa Video(VAR).

Kwa mujibu wa Bbc sports klabu hizo zinamuhitaji staa huyo lakini hazina budi kutoa kiasi cha paundi milioni 10 il kumsajili staa huyo aliyefunga mabao 25 msimu uliopita.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited