Home Soka Simba Sc Watua Znz

Simba Sc Watua Znz

by Sports Leo
0 comments

Msafara wa klabu ya Simba sc umewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya muda mfupi kujiandaa na mechi dhidi ya mtani wake wa jadi Yanga sc siku ya Jumamosi April 20 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc iliondoka mchana wa leo kuelekea Visiwani humo ambapo pia iliweka kambi ya aina hiyo ikijiandaa kuwakabili Al Ahly katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam na kufungwa 1-0.

Kambi hiyo ni mapendekezo ya kocha Abdelhack Benchika ambaye pamoja na kwamba anafanya jitihada zote za kufundisha mbinu mbalimbali bado mpaka sasa hajaridhishwa na ubora hasa wa safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kutokana na kukosa mabao ya wazi.

banner

Mchezo huo wa Jumamosi utatoa picha halisi ya mbio za ubingwa ambapo mpaka sasa Yanga sc yupo kileleni akimzidi Simba sc aliyeko nafasi ya tatu kwa alama tisa japo Simba sc ina mchezo mmoja mkononi na endapo Yanga sc atashinda basi pengo la alama litakua alama 12 na endapo Simba sc atashinda basi pengo la alama litakua 6 na Simba sc atakua na mchezo mmoja mkononi.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited