Home Soka Simba,Ajibu Kimeeleweka

Simba,Ajibu Kimeeleweka

by Sports Leo
0 comments

Taarifa za ndani ya klabu ya Simba Sc zinadai kuwa aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc Ibrahimu Ajibu Migomba tayari amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili ijayo na kinachosubiriwa ni kutambulishwa tu.

Mshambuliaji huyo mwenye kipaji cha hali ya juu inadaiwa amesaini mkataba huo siku moja na wachezaji wengine kama Jonas Mkude  kwa dau la milioni 85 na hata picha za utambulisho wake nguo alizovaa tajiri Mo dewji zinafanana na zile alizoonekana nazo wakati anamsainisha Mkude.

Ajibu ameendelea kukanusha taarifa za kujiunga na waajiri wake wa zamani na inasemekana amefanya mazungumzo na Yanga sc japo Sportsleo linafahamu hiyo ni danganya toto anayowafanyia wanajangwanin hao kwani tayari ameshamalizana na Wanamsimbazi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited