Home Soka Tshitshimbi,Ngassa Kuiongoza Yanga

Tshitshimbi,Ngassa Kuiongoza Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kocha Mwinyi Zahera amewateua Papy Kabamba Tshitshimbi na Mrisho Ngasa kuwa manahodha wapya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambayo timu hiyo itashiriki.

Zahera amefikia uamuzi huo kufuatia kuondoka kwa manahodha wa timu hiyo msimu uliopita Ibrahim Ajibu aliyesajiliwa na Simba sc na Thabani Kamusoko ambaye amejiunga na Zesco united chini ya kocha wa zamani wa Yanga George Lwandamina baada ya Yanga kumtema kwa kigezo cha majeraha na umri.

Awali inadaiwa nafasi hiyo ilibidi apewe Kelvin Yondani ambaye alinyan’ganywa awali kwa kigezo cha utovu wa nidhamu na nafasi hiyo kupewa Ajibu na inasemekana beki huyo mkongwe alikataa kurudishiwa cheo hicho.

banner

Tshitshimbi amepewa nafasi hiyo kutokana na kuonyesha kiwango bora katika msimu uliopita pia kuwa na mkataba mpya wa miaka miwili na kukosekana kwa wakongwe wenye vigezo mbali na Yondani kumembeba mkongo huyo huku Ngassa akiwa ameitumikia timu hiyo kwa muda mrefu katika vipindi tofautitofauti.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited