Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga, Cloutos Chama, na Shomary Kapombe wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya jumapili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha ndani ya klabu hiyo ni kwamba wachezaji hao tayari wamejulishwa kuhusu hilo huku ikibainika kwamba suala hilo linaweza kutangazwa ama kutotangazwa kwa umma lakini utekelezaji wake unaanza mara moja.
Simba sc ilikubali kipigo hicho siku ya jumapili novemba 5 huku mastaa hao wakiwa uwanjani ambapo wanatuhumiwa na uongozi kutokana na kuonyesha viwango duni kiasi cha kuruhusu mabao hayo.
Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimesema kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kuhusu tuhuma hizo ambapo kipindi chote cha uchunguzi mastaa hao watakua nje ya kambi ya timu hiyo.
Kipigo hicho cha mabao 5-1 kutoka kwa mahasimu wao wakuu Yanga sc kimezua kizaazaa klabuni hapo ambapo tayari kocha Roberto Oliveira na kocha wa viungo wametimuliwa.