Home Soka Eng.Hersi Afuata Mashine Congo DRC

Eng.Hersi Afuata Mashine Congo DRC

by Sports Leo
0 comments

Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said amesafiri kuelekea nchini Congo Drc kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji wawili ambao wanacheza nafasi za beki na winga kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo msimu ujao wa 2024/2025.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga sc zinadai kwamba Hersi amekwenda kufanya usajili huo kwa ajili ya kuziba nafasi ya Mahalatse Makudubela na Joyce Lomalisa Mutambala ambao klabu hiyo itaachana nao mwishoni mwa msimu huu.

Wanaotajwa kusajiliwa na Hersi nchini humo ni winga wa klabu ya Tp Mazembe Philipe Kinzubi na beki wa Fc Lupopo Chadrack Boka ambao kama mambo yataenda sawa basi wataichezea Yanga sc msimu ujao ambapo wote wawili viwango vya vimewavutia mabosi wa klabu hiyo.

banner

Boka ambaye ametimiza miaka 24 msimu huu amekua moto wa kuotea mbali nchini humo akiwa ni moja ya walinzi bora wa kushoto katika ligi kuu ya Congo Drc huku klabu za Tp Mazembe,Petro de Luanda na Wydad Ac ni miongoni mwa Vilabu vilivyokuwa vinafikifiria kuipata saini mwishoni mwa Msimu huu.

Utofauti wake na Joyce Lomalisa ni uwezo kupandisha timu kwa kasi na kurejea kwenye nafasi yake kwa wakati huku akisifika kwa kupiga vizuri mipira ya kutenga kama faulo ama penati ambapo ana uwezo wa kuchangia upatikanaji wa mabao kuanzia kumi kwenda juu.

Kocha Miguel Gamond anaonekana hajaridhishwa na kiwango cha Skudu Makudubela huku Lomalisa akiwa hana nia ya kusalia jangwani ndio maana klabu imeamua kutafuta mbadala ambapo tayari pia Nickson Kibabage akiwa ameongeza mkataba wa miaka mitatu kusalia klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited