Home Makala Kagera Sugar Fc Mbioni Kumtema Mganda

Kagera Sugar Fc Mbioni Kumtema Mganda

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Kagera Sugar Fc ya mkoani Kagera ipo katika hatua za mwisho kuachana na kocha wake mkuu paul Nkata raia wa Uganda kutokana na matokeo yasiyoridhisha katika michuano ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Nkata aliyejiunga na Kagera Sugar Fc msimu huu wa ligi kuu mpaka sasa amekiongoza kikosi hicho katika michezo saba ya ligi kuu ambapo wameshinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare mchezo mmoja huku wakifungwa michezo mitano na kuambulia alama nne kati ya 21.

Nkata anaondolewa sambamba na wasaidizi wake wote ambapo inatarajiwa kuwa klabu hiyo kuajiri benchi zima la ufundi.

banner

Kocha huyo sasa anaungana na makocha Yousouph Dabo wa Azam Fc,Goran Kapunovic wa Pamba jiji katika orodha ya makocha wa ligi kuu waliotulimuliwa mapema zaidi.

Tayari kocha huyo ameshapewa taarifa za kusitishwa kwa mkataba wake ambapo sasa anasubiri taratibu za kiutawala kukamilika ili kuachana rasmi na klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited