Stars Kuweka Kambi Nchini Misri

stars kuweka kambi Misri - sportsleo.co.tz

Kikosi cha timu ya Taifa Stars imesafiri kuweka kambi nchini Misri alfajiri ya leo  Julai 09 baada ya jana Julai 8 kuingia kambini jijini Dar es salaam kujiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) itakayofanyika katika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda.

Taifa Stars Agosti 02 2025 itacheza mechi ya Ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024 dhidi ya Burkina Faso katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo mwishoni mwa mwezi huu kikosi kitakua kimerejea nchini kwa ajili ya mchezo huo.

Mpka kufikia leo Julai 09 2025 zimebaki siku 25 kwa ajili ya hayo mmashindano hayo ya CHAN huku Tanzania ikipewa heshima ya kuwa na makundi mawili visiwani Zanzibar na jijini Dar Es Salaam.

Mpaka sasa Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema kuwa maandalizi muhimu kuelekea mchezo huo wa ufunguzi yapo tayari huku vikisalia vitu vichache ambavyo vinaendelea kufanyiwa kazi kwa Ushirikiano wa karibu na serikali.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks