Kiungo wa Shoka Asajiliwa Yanga Sc

Karibu Jangwani Karibu Jangwani, Abdulnassir Mohamed,Umesomeka ujumbe ulioandikwa katika mitandao ya kijamii ya klabu ya Yanga sc wakimtambulisha kiungo huyo kutoka Mlandege Fc ya Zanzibar.
Yanga sc imekamilisha usajili wa kiungo huyo wa ulinzi kinda kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Jonas Mkude ambaye ametemwa klabuni hapo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza.
Mabosi wa Yanga sc walivutiwa na mchezaji huyo baada ya kumuona katika kombe la Muungano Visiwani Zanzibar na kuwavutia kutokana na kuonyesha kiwango bora kabisa.
Yanga sc wanaona bora wachukue damu changa ambaye atakua msaada kwa timu kwa muda mrefu na kuachana na Mkude ambaye alishindwa kuwavutia makocha zaidi ya watatu waliofundisha klabu hiyo kwa nyakati tofauti wakianza na Miguel Gamondi,Sead Ramovic kisha Miloud Hamdi ambao wamedumu kwa muda klabuni hapo.
Kiungo huyo ana sifa za kucheza kama kiungo wa ulinzi ambapo sasa analazimika kujifunza kwa Moussa Balla Conte ambaye atakua anapata nafasi mara kwa mara.
