Fadlu Amnasa Rushine

Kocha wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis amefanikiwa kumshawishi beki Rushine De Reuck kujiunga na klabu ya Simba Sc kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Mamelod Sundowns.
Fadlu anaamini beki huyo atatibu matatizo ya ulinzi klabu hapo ambapo mara kadhaa Che Malone Fondoh amekua na makosa ya mara kwa mara ya kiulinzi.
Kocha Fadlu Davids alishawahi kumfundisha Rushine De Reuck wakati anafundisha Maritzburg United ya Afrika kusini ambapo beki huyo pia alishawahi kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu Afrika kusini mwaka 2022.
Mpaka sasa mchezaji mpya wa Simba Sports Club na anaweza kumudu kucheza nafasi tatu uwanjani kama Mlinzi wa Kati, Mlinzi wa Kulia na Kiungo Mkabaji.
Beki huyo ataungana na mabeki Abdulrazak Hamza na Chamou Karabou kama mabeki wa kati wa kikosi cha Simba Sc kwa msimu ujao.
