Kiptoo Ashinda Athens Marathon

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Edwin Kiptoo ameshinda tuzo katika mbio za 40 za has won Athens Marathon kwa kuvunja rekodi akikimbia kwa kutimua masaa mawili na dakika kumi na sekunde thelasini na nne pekee.
Mwanariadha huyo mwenye miaka 30 aliwashangaza wengi baada ya kukimbia kilomita kumi pekee katika sehemu ya pili ya mbio hizo maarufu duniani huku wakati akimalizia mstari wa mwisho kumaliza mbio hizo zaidi ya mashabiki mia moja walionyesha bendera ya kuisapoti Palestina katika vita inayoendelea na Israeli ambapo bendera hizo zilisomeka “Free Palestine”.
Nafasi ya pili pia ilienda nchini Kenya ambapo Rhonzai Lokitam Kilimo alishika nafasi hiyo baada ya kutumia muda wa 2:12:36 na Felicien Muhitira wa Rwanda alikua wa tatu akitumia muda huo huo.
Wanariadha hao kutoka Kenya wameshinda kwa mara ya 17 tangu 2001 akiwemo Felix Kandie, ambaye aliweka rekodi hapo awali akitumia muda wa 2:10:37 mwaka 2014.

