Kisa Fei Waarabu Washusha Mabilioni Azam Fc

582617301 18539044789052678 423224590593356099 n

Klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya imebadili kabisa upepo wa usajili barani Afrika baada ya kutupia mezani ofa nono ya Dola za Marekani milioni 2 (takribani Sh bilioni 4.8) kwa ajili ya kumsajili kiungo mahiri wa Azam FC, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto. Hii ni ofa iliyokuja kwa kasi ya ajabu na kuibua mjadala mzito ndani ya anga la soka la Tanzania na Libya.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka kwa watu wa karibu na dili hilo, Al Ahly Tripoli wametuma ofa yao mpya usiku wa kuamkia leo, ikiwa ni mara ya pili kujaribu kumvuta kiungo huyo wa Taifa Stars. Ofa ya kwanza ya dola 800,000 ilikataliwa papo hapo na uongozi wa Azam FC kwa kile kilichoelezwa kuwa “haitoi thamani halisi ya mchezaji”.

Kisa Fei Waarabu Washusha Mabilioni Azam Fc-www.sportsleo.co.tz

Lakini Waarabu wa Libya hawakukata tamaa. Safari hii wamerudi na mzigo mzito uliowafanya wengi ndani ya Azam FC kukaa na kufikiri mara mbili. Ofaa ya dola milioni 2 imekuja ikiwa na masharti mepesi na dhamira ya kumaliza dili bila kupoteza muda. Habari zinaeleza kuwa Tripoli wako tayari kulipa fedha hizo haraka sana, bila kusubiri dirisha la mwisho wala vipengele virefu vya mazungumzo.

Mbali na kiasi cha pesa, Tripoli pia wameonyesha heshima kwa Azam FC kwa kuongeza kipengele kingine muhimu cha asilimia 10 ya mauzo ya baadaye endapo watamuuza Fei Toto kwenda klabu nyingine nje ya Libya. Hiki ni kipengele ambacho klabu nyingi barani Afrika hukipenda, kwa kuwa kinaongeza kipato cha muda mrefu na kuonyesha heshima kwa klabu inayomlea mchezaji.

Kwa upande wa mchezaji mwenyewe, chanzo chetu makini kimeeleza kuwa Fei Toto yuko tayari kabisa kuondoka Azam FC na kujiunga na Waarabu hao. Imeelezwa kuwa mazungumzo ya upande wa mchezaji na Tripoli yameshaanza kupiga hatua kubwa, huku Fei akiahidiwa signing-on fee kubwa mno pamoja na mkataba wa miaka mitatu wenye thamani inayokadiriwa kuvuka Sh.bilioni 10 ukijumuisha mshahara na malipo ya usajili.

Kisa Fei Waarabu Washusha Mabilioni Azam Fc-www.sportsleo.co.tz

“Fei ameshavutiwa na mpango mzima,” kinadokeza chanzo. “Kile alichopangiwa ni fedha ambazo mchezaji yeyote wa Tanzania angezitaka. Tripoli wameonyesha kwamba wanamtaka sana na wako tayari kumthamini anavyostahili.”

Kwa upande wa Azam FC, japo bado hawajaweka wazi msimamo wa mwisho, taarifa zinasema kuwa kuna mjadala mkubwa ndani ya uongozi kuhusu kama wamruhusu nyota wao huyo kuondoka sasa au wasubiri hadi msimu ujao. Fei amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu ndani ya Azam, hivyo huu ndio wakati ambao wanaweza kupata dau kubwa kabla ya mkataba wake kuingia mwaka wa mwisho ambapo thamani yake inaweza kushuka.

Fei, ambaye pia ni sehemu ya kikosi cha Taifa Stars, amekuwa mmoja wa viungo bora zaidi nchini katika miaka ya karibuni. Anasifika kwa kasi, ujasiri wa kumiliki mpira, uwezo wa kupenya katikati ya uwanja na pasi za mwisho zenye macho mawili. Ubora huo ndio uliowafanya Waarabu kutaka kumleta Libya kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kinachowania ubingwa wa ndani na pia nafasi nzuri kwenye mashindano ya CAF.

Huku mashabiki wa Azam wakisubiri taarifa rasmi, hali ni tete. Baadhi wanaamini Fei anastahili kwenda kutafuta maslahi na changamoto mpya, huku wengine wakihofia pengo atakaloliacha pale Chamazi. Wengi wameanza kujadili mitandaoni, wakijiuliza kama Azam watamshikilia kwa gharama yoyote au watafungua mlango na kuhesabu mabilioni yao mapya.

Mpaka sasa, Al Ahly  Tripoli wanaonekana hawataki masihara. Wametuma ofa, wako tayari kulipa mara moja, wameweka kipengele cha asilimia 10, na wamempa Fei ahadi ya maisha mapya yenye malipo makubwa. Uamuzi sasa uko mikononi mwa Azam FC kubaki na nyota wao au kuvuna mamilioni ya dola.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks