Home Makala Kibwana Shomari Asalia Yanga sc

Kibwana Shomari Asalia Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu ya Yanga sc Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelee kuitumikia klabu hiyo baada ya ule wa awali kuelekea mwishoni aliousaini akitokea klabu ya Mtibwa Sugar miaka miwili iliyopita.

Mchezaji huyo mwenye miaka 21 amekua mchezaji tegemea klabuni hapo akichezeshwa sehemu ya beki wa pembeni kushoto ama kulia sehemu ambazo ameonyesha uwezo mkubwa sana hasa katika kukaba.

Kibwana ameonekana kupitia kipande cha video katika mtandao wa youtube wa klabu hiyo akithibitisha kusalia klabuni hapo kwa miaka miwili zaidi.

banner

”Nipo ndani ya Yanga kwa sasa na hii ni habari nzuri kwa wengi ambao wanapenda mimi kuwa hapa kwa Wananchi kuendelea kufanya kazi.

“Kwa wale ambao hawapendi nina amini kwamba itawauma basi wakae kimya na kwa sasa nipo ndani ya Yanga kama Wananchi wamenitaka mimi nani niweze kukataa kusaini Yanga?Alisema Kibwana

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited