Home Makala Musonda,Yao Fiti Kuwavaa Singida Fg

Musonda,Yao Fiti Kuwavaa Singida Fg

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi amethibitisha kurejea kwa wachezaji Kennedy Musonda na Yao Kouasi baada ya kuwa majeraha yaliyosababisha wakosekane katika michezo kadhaa ya ligi kuu nchini.

Musonda amekosekana kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Ihefu FC, Geita Gold na Azam FC huku Yao akikosekana katika mchezo wa juzi dhidi ya Azam Fc ambapo Yanga sc iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Kurudi kwa mastaa hao kunatoa wigo mpana kwa Gamondi kupangilia kikosi chake kuelekea mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa Oktoba 27 ambapo kitalazimika kupata alama tatu ili kujichimbia kileleni kwani mchezo unaofuatia watakutana na Simba sc Novemba 5.

banner

Kwa mujibu wa kocha huyo tayari Musonda amepona na ameshiriki program za mazoezi kikamilifu kabisa huku pia Yao akisema kuwa amepona kabisa majeraha ya enka yaliyokua yakimsumbua na sasa anaendelea vizuri.

“Tayari ameshaanza mazoezi tangu Jumapili iliyopita lakini sikuona sababu za kumtumia dhidi ya Azam FC kutokana na kuhofia kumpa presha na akapata shida nyingine nikampa mapumziko.” alisema kocha Gamondi raia wa Argentina

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited