Home Makala Simba Sc Yajipoza Kwa Coastal Union

Simba Sc Yajipoza Kwa Coastal Union

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imejipoza kutoka kufungwa Derby ya kariakoo na Yanga sc baada ya kuibamiza Coastal Union kwa bao 1-0 katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu ya Ngao ya Jamii uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo kocha Fadlu Davis aliamua kuanza na wachezaji wanne wapya kutoka katika kikosi kilichocheza dhidi ya Yanga sc akiwaanzisha Salehe Karabaka,Abdulrazak Hamza,Augustine Okejepha na Kelvin Kijiri huku golini akianza na kipa yule yule Mohammed Camara.

Iliwachukua Simba sc dakika 10 kupata bao pekee katika mchezo huo lililofungwa na Karabaka akimalizia pasi nzuri ya Steven Mukwala aliyemzidi maarifa beki wa Coastal Union.

banner

Pamoja na kumiliki mchezo huo bado Simba sc walishindwa kutumia nafasi za wazi zilizopatikana hasa Mukwala na Karabaka waliokosa nafasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili.

Kocha David Ouma aliamua kuwapumzisha mastaa watano kutoka kikosi kilichofungwa 5-2 na Azam Fc huku golini akimuanzisha Ramadhan Chuma na kumuweka Athuman Msekeni benchi sambamba na Felly Mulumba huku Gerson Gwalala akiingia kipindi cha pili.

Simba sc wamepata medali ya mshindi wa tatu kwa wachezaji ambao walivalishwa baada ya mchezo wa fainali wa Yanga sc dhidi ya Azam Fc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited