Mikeka Yaipa Mabilioni Serikali

Screenshot 20250604 193648 Instagram

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2025, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania imekusanya jumla ya Tsh. bilioni 17.42, sawa na asilimia 70 ya lengo la mwaka na imefanya programu tatu za kuelimisha jamii juu ya michezo ya kubahatisha, faida na hasara pamoja na dhana nzima ya kucheza kwa kiasi (responsible gaming).

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2025 Waziri huyo mwenye dhamana ya fedha ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba  magharibi alisema kuwa

“Kwa mwaka 2024/25, Bodi ilipanga kutoa leseni 12,456 ikijumuisha leseni mpya 1,126 na kuhuisha leseni 11,330, kufanya kaguzi 12 kwa kuzingatia vihatarishi, kutekeleza operesheni nne za kudhibiti michezo haramu ya kubahatisha, kukusanya mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha ya jumla ya shilingi bilioni 24.89”.

Mbali na kuingiza faida hiyo pia alisema kuwa bodi imeendelea kutoa elimu juu ya michezo ya kubahatisha ambapo wananchi wanakumbushwa kucheza kwa kiasi.

“kuhusu kuelimisha jamii kuhusu athari hasi za michezo ya kubahatisha na kusimamia uendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa hadi kufikia April 2025, Bodi imetoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu madhara ya kubashiri ambapo jamii imeaswa kucheza kwa kiasi”Alisema Mh.Mwigulu

Tanzania imekua moja ya nchi zilizoibuka kwa kasi katika michezo ya kubashiri kuanzia mwaka 2016 ambapo kampuni mbalimbali za kubashiri ziliingia nchini na kuilazimu serikali kutunga sheria mbalimbali za kusimamia mchezo huo.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks