Nyota wawili wa Yanga Ditram Nchimbi na Feisal Salum wanatarajiwa kuelekea nchini Misri kufanya majariboio kunako klabu ya Smouha inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo
Nyota hao huenda wakaondoka Januari 27 baada ya mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la Azam kati ya Yanga dhidi ya Prisons ambao utapigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa
Inaelezwa kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ndiye aliyezuia kuondoka kwa wachezaji hao mapema licha ya kuwa taratibu zao za safari zilikuwa zimekamilishwa