Home Soka Yanga Hakuna Kulala

Yanga Hakuna Kulala

by Sports Leo
0 comments

Baada ya mchezo dhidi ya Alliance Fc, ligi itasimama kupisha michuano ya CECAFA Chalenji ambayo itafanyika nchini Uganda kuanzia Disemba Mosi

Kulingana na ratiba ya Bodi ya Ligi, baada ya michuano ya CECAFA Chalenji kumalizika, mchezo utakaofuata ni Yanga dhidi ya Simba January 04 2020.

Lakini mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itaifuata Alliance Fc Novemba 29 jijini Mwanza kucheza moja ya mechi zake za viporo kabla ya baadhi ya wachezaji wake kwenda kujiunga na timu za Taifa kushiriki michuano hiyo

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema timu itaendelea na mazoezi kipindi chote cha mapumziko hayo

Aidha amesema watawajumisha kwenye kikosi baadhi ya nyota ambao wanataka kuwasajili dirisha dogo kujiridhisha na uwezo wao

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited