Stars Kambini Kuivaa Sudan

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) kimeingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Sudan unaotarajiwa kufanyika siku ya Oktoba 18 ambapo mchezo huo utafanyika nchini Saudin Arabia.
Licha ya kikosi hicho kutowekwa hadharani lakini picha za mitandao zimewaonyesha mastaa kama Dickson Job,Nickson Kibabage,Bakari Mwamnyeto,Ibrahim Hamad,Metacha Mnata na Clement Mzize kutoka Yanga sc huku Kibu Dennis na Mzamiru Yassin kutoka Simba sc nao wakionekana katika picha hizo zilizowekwa katika mitandao ya Shirikisho la soka nchini(TFF).
Wengine walionekana ni George Mpole kutoka Fc Lupopo,Saimon Msuva,Novatus Dismas,Sospeter Bajana,Baraka Majogoro pamoja na mastaa wengine.
Kocha Adel Amrouche ameamua kutotangaza kikosi kinachoingia kambini ambapo inasemekana lengo la kufanya hivyo ni kuepuka mijadala kutoka kwa waandishi wa habari ambao mara kadhaa wamekua wakizua mijadala hasa baada ya siku za hivi karibuni kocha huyo kuwatema Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kutoka Simba sc.
