Tanzania Prisons Yaachana na Josia

Screenshot 20250710 165631 Instagram 1

Klabu ya Tanzania Prisons Yaachana na Josia  Amani Josiah aliyekua kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kutokanan na makubaliano ya pande mbili baada ya kuwa na msimu mbaya wa ligi kuu na kombe la Shirikisho la Crdb nchini.

Kocha huyo aliyechukua nafasi ya Mbwana Makata ambaye hapo awali alitimuliwa kutokana na matokeo mabaya ya timu na kuletwa Josiah ili kuokoa jahazi la timu hiyo ambapo amefanikiwa kuibakisha ligi kuu japo kwa mbinde.

Prison na Josiah wameachana kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya klabu hiyo kutokupata matokeo mazuri katika msimu uliopita 2024/25 kwa kushika nafasi ya 13 ya msimamo wa Ligi Kuu hali iliyowafanya kwenda kucheza michezo ya mtoano ambapo waliwatoa Fountain Gate Fc.

Sasa mabosi wa Prisons wanaangalia uwezekano wa kuajiri kocha mpya ili aweze kufanya usajili wa maana kuelekea msimu ujao.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks