Yanga Sc Yasajili Kiungo wa Zanzibar

Klabu ya Yanga sc imehamia Visiwani Zanzibar kwa muda baada ya kumsajili na kumtambulisha kiungo Abubakar Nizar ambaye amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu.
Yanga sc imekamilisha usajili wa kinda huyo ambaye atakua na nafasi ya kucheza kikosi cha vijana na mara kadhaa atafanya mazoezi na timu ya wakubwa ili kuendelea kupata uzoefu zaidi.
Nizar maarufu kama Ninju ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za kiungo wa ukabaji pamoja na beki wa kati akiwa na uzoefu kutoka katika timu ya vijana ya Azam Fc.
Lengo kuu la klabu ya Yanga sc msimu ujao licha ya kuwa na timu nzuri ya wakubwa pia wana mpango wa kuwa na timu nzuri ya vijana ambao baadhi watakua na uzoefu wa kufanya mazoezi na timu ya wakubwa.
Mabosi wa Yanga sc wanaamini pia vijana hao watakua na mchango mkubwa siku zijazo huku pia wakifanya biashara ya kuwauza endapo zitakuja ofa nzuri zaidi.
Ninju anaungana na Casemiro ambao wote watakua wamesajili kutokea visiwani Zanzibar msimu huu.

