Pacome Atia Fora Caf

407834194 912161166936482 8660971059517501969 n

Bao la kusawazisha alilolifunga kiungo wa Yanga Sc Pacome Zouzoua katika mchezo dhidi ya Al Ahly limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoendelea barani Afrika.

Pacome alifunga bao hilo akipokea pasi ya Kennedy Musonda na kuifanya klabu yake ya Yanga sc kupata alama moja katika mchezo huo uliokua mkali na wa kusisimua uliofanyika Jumamosi Disemba 2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kilichofanya bao hilo likachaguliwa na Caf kuwa bao bora ni namna lilivyopatikana ambapo Pacome alifunga akiwa katikati ya mabeki watatu wa Al ahly huku pia akiwa ameanzisha yeye mwenyewe shambulizi hilo kuelekea ndani ya eneo la hatari.

Ni utaratibu wa Caf kila wiki kutangaza bao bora baada ya kuchezwa mechi za makundi ambapo bao lililopatikana kwa kuundwa kwa shambulizi zuri ndio huchaguliwa.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks