Aucho Yupo Sana Yanga Sc

Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc imemaliza utata kuhusu hatma ya kiungo wake mkabaji Khalid Aucho kwa kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja na Sasa Aucho Yupo Sana Yanga Sc baada ya mkataba wake kuelekea ukingoni msimu huu.
Chanzo chetu kutoka klabuni humo kimesema kuwa licha ya makali ya kiungo huyo kuanza kupungua kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara bado mabosi wa klabu hiyo wameona umuhimu wa kuendelea kusalia nae kikosini.
“Tunaheshimu mchango wa Aucho ambaye uzoefu wake unaonekana uwanjani, hivyo uwepo wake, kuna kitu kikubwa kitaendelea kuongezeka katika eneo la kiungo”,kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo.
Huu ni msimu wa nne kwa kiungo huyo tangu ajiunge na klabu hiyo msimu wa 2021-2022 ambapo amefanikiwa kuifanya safu ya kiungo ya klabu hiyo kuwa imara ambapo sasa wametwaa mataji ya ligi kuu na kombe la Shirikisho mara nne mfululizo.
