Azamtv Yaibuka Kidedea Kesi ya Vitasa

Screenshot 20250526 225136 Instagram

Mahakama Kuu ya Tanzania imeipa ushindi Azam Media Limited katika kesi ya madai ya haki miliki iliyofunguliwa na bondia Amos Mwamakula kutokana na kampuni hiyo kutumia wazo la mashindano ya ngumi maarufu kama “Vitasa”.

Awali, Mahakama ya Kinondoni iliiamuru Azam Media Limited kumlipa bondia huyo kiasi cha shilingi milioni 250, baada ya kudai kuwa kampuni hiyo ilichukua wazo lake la kipindi cha “Boxing Kazi Kazi” kinachohusu masuala ya ndondi na kukitumia kwa jina la “Vitasa”.

Baada ya hukumu hiyo kampuni hiyo ilikata rufaa katika Mahakama kuu nchini ikiomba marejeo ya uamuzi kwani haikuridhika ambapo baada ya miezi kadhaa leo uamuzi umetolewa na Azam Media kupewa ushindi.

Mahakama Kuu baada ya kusikiliza shauri hilo imeipa ushindi Azam Media Limited kwa kuzingatia sheria za hati miliki.

Wakili Neema Mbaga anayewakilisha Azam Media, amesema ushindi huo unaiwezesha Azam TV kuendelea na shughuli zake za kurusha vipindi vinavyohusiana na ndondi na mapambano mbashara ya ndondi.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks