Mlandege Yatinga Fainali Mapinduzi Cup

Snapinsta.app 418369024 1440219183196315 7176692263286068402 n 1080

Mlandege FC imefuzu hatua ya fainali Mapinduzi Cup 2024 baada ya kuitoa APR ya Rwanda kwa penalti 4-2 kwenye mechi ya nusu fainali iliyoisha dakika 90 bila kufungana (0-0) na wenyeji kufanikiwa kushinda kwa penati.

Kipa wa Mlandege Fc Othmani Hassan aliibuka shujaa kwa klabu yake baada ya kufanikiwa kudaka michomo miwili ya penati ikiwemo ile ya kistaa iliyopigwa na Sharaff Eldin Shiboub ambaye amejizolea umaarufu katika michuano hiyo kutokana na kuonyesha kiwango kizuri.

Michuano hiyo imekua maarufu visiwani Zanzibar kutokana na kufanyika mwezi januari ambapo timu nyingi zimekua na kawaida ya kufanya usajili wa mastaa ambao moja kwa moja huonekana katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Mlandege ndiyo mabingwa watetezi wakibeba kombe hilo mbele ya Singida Fountain Gate ambayo  imetolewa na Simba sc  katika nusu fainali ya pili saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks