Namungo Fc Waanza Na Kocha Mgunda

Uongozi wa klabu ya Namungo Fc umeanza na Kocha Juma Mgunda katika kusafisha kikosi hicho kuelekea msimu ujao kwa kumtema yeye pamoja na benchi lake la ufundi lote.
Uongozi wa timu hiyo umeamua kuanza upya kwenye benchi lao la ufundi kwa kuachana na makocha wake wote watatu kocha muu Juma Mgunda, Kocha msaidizi Ngawina Ngawina na Shadrack Nsajigwa ambapo sasa linakuja benchi jipya love.
Hata hivyo kocha Juma Mgunda ataendelea kusalia kama kocha msaidizi wa Taifa Stars na sasa yupo nchini Misri kujiandaa na mashindano ya CHAN 2024 Ambapo baadhi ya michezo itachezwa hapa nchini ukiwemo mchezo wa ufunguzi.
Kwa upande wa makocha wasaidizi Ngawina Ngawina na Nsajigwa wenyewe sasa wanapaswa kuangalia fursa katika klabu zingine za ligi kuu kwa kuwa ni maisha ya kawaida kwa makocha kuondoka katika timu.
Msimu ulioisha wa ligi kuu ya Nbc nchini timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tisa ikikusanya alama 35 katika michezo 30 ya ligi kuu nchini.
