Simba sc Yashinda 6-0

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuifunga timu ya Tra Moshi kwa mabao 6-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.
Simba sc iliandika bao la kwanza dakika ya 13 likifungwa na Ladack Chasambi aliyepokea pasi kutoka kwa Fred Michael huku Sadio Kanoute akifunga mabao mawili dakika za 40,52 huku pia Fred Michael nae akifunga dakika za 51 na 55.
Pa Omar Jobe naye hakua nyuma ambapo alifunga bao la sita dakika ya 72 ya mchezo na kukamilisha idadi hiyo ya mabao huku Simba sc ikifuzu hatua inayofuatia ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Azamtv.
Kocha Abdelhack Benchika pia alimuingia kiungo mpya wa klabu hiyo Edwin Balua ambaye alisajiliwa kutokea Tanzania Prisons huku pia Duchu naye akicheza katika beki ya kulia kwa dakika zote tisini.

