Mayele Aomba Kuondoka Pyramids

34B294EE 4BF0 4732 92FE 15F5F7E7B542

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Fiston Mayele  amewasilisha barua kwenye Menejiment ya klabu ya Pyramids  kwa ajili ya kuhitaji kusitishiwa mkataba wake ili akapate changamoto mpya sehemu nyingine.

Taarifa kutoka ukurasa wa  Michezo wenye makazi yake Saudi Arabia Zoal_Sport imeripoti kuwa Fiston Kalala Mayele ameomba kusitisha mkataba wake na klabu hiyo kutokana na kutopata nafasi zaidi huku akipungua makali yake ya kufunga.

Mayele anaona kwamba mfumo wa timu hiyo haumpi nafasi nzuri ya kufunga tofauti na alivyokua na Yanga sc ambapo mpaka sasa katika ligi kuu ya Misri amecheza michezon tisa na kufunga mabao manne huku katika ligi ya mabingwa Afrika akicheza michezo sita na hajafunga goli na katika michuano ya kombe la shirikisho la Misri amecheza mchezo mmoja na hajafunga.

Takwimu hizo za Mayele ni tofauti na msimu uliopita ambapo akiwa Yanga sc alifunga jumla ya mabao 17 ya ligi kuu huku akiibuka mfungaji bora wa kombe la shirikisho msimu uliopita.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks