Home Soka Ivory Coast hao Fainali

Ivory Coast hao Fainali

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kuanza kwa kusuasua kamamwenyeji katika michuano ya mataifa ya Afrika timu ya Ivory Coast imefanikiwa kufuzu hatua ya Fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga DR Congo kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali.

Licha kupiga mashuti 14 langoni mwa Congo DR ni mashuti mawili tu yalilenga lango na moja kuwa goli lilifungwa na Sebastien Haller dakika ya 65 ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo licha ya Congo kupiga mashuti 7 ambapo mawili yalilenga lango.

Katika muda wa dakika tisini za mchezo huo wenyeji walitawala mchezo wakipiga jumla ya pasi 377 dhidi ya 278 za DRC ambapo walitawala mchezo kwa asilimia 57 japo walikosa umakini katika matumizi ya nafasi.

banner

Maajabu katika mchezo ni nidhamu kwa pande zote mbili ambapo hakukua na kadi ya aina yeyote huku Ivory Coast watakutana na Nigeria katika hatua ya fainali ya michuano hiyo siku ya Jumapili saa tano usiku kwa saa za Tanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited