Home Soka Niyonzima- “bye bye”Simba

Niyonzima- “bye bye”Simba

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Mnyarwanda wa Simba sc Haruna Niyonzima ameaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya kutopewa mkataba mpya na klabu hiyo baada ya mkataba wa awali kumalizika msimu huu.

Kiungo huyo fundi alijiunga na Simba sc mwaka 2017 akitokea kwa mahasimu wao wa jangwani Yanga sc kwa dau linakadiliwa zaidi ya shilingi milioni 100 za kitanzania.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya mchezaji huyo ametuma ujumbe wa kuaga kwa mashabiki wa klabu hiyo huku akitangaza kwamba muda si mrefu ataweka bayana timu atakayoitumikia msimu ujao japo tetesi zinasema matajiri wa chamazi Azam Fc wanaweza kumsajili mchezaji huyo .

banner

Hata hivyo inaripotiwa kuwa Simba ilikua tayari kumpa mkataba mchezaji huyo lakini kulitokea kutoelewana katika baadhi ya vipengele vya mkataba hasa dau la usajili na mshahara.

Niyonzima ni moja ya wachezaji wa kigeni wenye mafanikio zaidi akitwaa ubingwa wa ligi kuu mara tano mfululizo tatu mfululizo akiwa Yanga na mara mbili mfululizo akiwa na Simba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited