Ushirikina Wamponza Kyombo

Snapinsta.app 370040403 336888252358789 6575153923027457157 n 1080

Mshambuliaji wa Singida BS, Habibu Kyombo ametozwa faini ya Tsh milioni moja kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina katika mchezo kati ya Singida Fontaine Gate FC dhidi ya Namungo FC.

Kyombo alionekana akimwaga kimiminika katika goli la klabu ya Namungo katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Majaliwa, Ruangwa na kumalizika kwa ushindi wa 3-2 kwa Singida Fontaine Gate FC.

Bodi ya ligi nchini imetoa adhabu hiyo kwa mshambuliaji huyo kwa kuzingatia kanuni ya 41:5(5.5) ya ligi kuu ambayo inahusu udhibiti wa wachezaji.

Kyombo mshambuliaji wa zamani wa Mbao Fc na Simba sc amekua na kiwango kizuri siku za hivi karibuni akitupia magoli mawili katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc uliofanyika katika uwanja wa liti mkoani Singida.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks