Yanga Sc Yatwaa Ubingwa Mbele ya Simba Sc

Klabu ya Yanga Sc Yatwaa Ubingwa Mbele ya Simba Sc baada ya kupata alama tatu katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba Sc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Yanga sc ilipaswa ama kushinda au kutoa sare kupata ubingwa huo huku Simba sc ikipaswa kushinda ili kuizidi Yanga sc kwa alama 2 zaidi ili kutwaa ubingwa ambao umechukuliwa na Yanga sc mara tatu mfululizo.

Dalili za ubingwa kwa Yanga sc zilionekana mapema punde tu mchezo ulipoanza ambapo walikua imara katika eneo la kiungo wakiwachezesha kwa pamoja Duke Abuya,Khalid Aucho na Mudathir Yahaya ambao waliwafunika Fabrice Ngoma na Yusuph Kagoma katika eneo hilo.
Prince Dube hakua na wakati mzuri akikosa ufanisi mara kadhaa huku ikionekana kama hajapona sawasawa maumivu ya nyama za paja aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Kuingia kwa Clement Mzize kipindi cha pili kulibadili muundo wa ushambuliaji wa Yanga sc na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 66 kupitia kwa penati iliyopigwa kiufundi na Pacome Zouzoua dakika ya 66 ya mchezo.

Yanga sc waliendelea kutawala mchezo huo huku Simba Sc wakionekana hawana mipango ya kusawazisha bao hilo licha ya kuingia kwa Lionel Ateba,Abdulrazak Hamza na Awesu Awesu ambao pia walikosa mipango ya mabao.
Kalamu ya mwisho ilihitimishwa na Clement Mzize dakika ya 85 baada ya kufunga bao la pili kwa Yanga sc akipokea pasi nzuri ya Pacome Zouzoua na kumchungulia kipa Moussa Camara aliyekua hana la kufanya.
Pamoja na burudani hiyo uwanjani pia burudani nyingine ilikua kwa mwamuzi raia wa Misri Mohammed Amin namna alivyoumiliki mchezo huo na kutoa maamuzi sahihi kila wakati ambayo kila mtazamaji aliridhika na uamuzi.
Yanga sc sasa imetwaa ubingwa wa 31 kwa jumla na mara nne mfululizo na sasa ni moja ya timu bora kabisa hapa nchini na Afrika mashariki kwa ujumla.
