Singida FG Yahamia Karatu

Snapinsta.app 408163003 18207880882276348 8949866301890432886 n 1080

Klabu ya Singida Fountain Gate itautumia uwanja wa Black Rhino Academy uliopo karate,Arusha kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani baada ya kufungiwa kwa uwanja wake wa nyumbani wa  Liti ulioko mkoani Singida.

Uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vyenye nyasi asilia ambavyo ni bora hapa nchini huku eneo lake la kuchezea likiwa na ubora mkubwa kama viwanja vingine vikubwa nchini ikiwemo Benjamini Mkapa ulioko jijini Dar es salaam.

Hivi karibuni bodi ya ligi kuu nchini ilitangaza kuufungia uwanja wa Liti kutokana na kuwa na miundombinu iliyochakaa ikiwemo eneo la kuchezea huku timu hiyo ikiambiwa kwa sasa itafute uwanja mwingine kwa muda kupisha matengenezo ya uwanja huo.

Mara kadhaa timu mbalimbali za Taifa zimekua zikiweka kambi katika uwanja huo huku Singida FG nao mwanzoni mwa msimu waliweka kambi ya maandalizi ya msimu katika uwanja huo.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks