Kinda wa kituruki Kenan Yildiz alifunga mabao mawili ambapo akiongoza Juventus ikipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika Kombe la Dunia la Klabu (Club World Cup) Jumapili hii kuifanya klabu hiyo kukaribia kufuzu kwenye raundi ya 16.
Timu hiyo ya Italia iko kwenye nafasi ya kwanza ya Kundi G kwa alama sita baada ya mechi mbili alama tatu mbele ya Manchester City, ambayo itacheza dhidi ya Al Ain ya UAE mapema Jumapili usiku.
Juventus itafuzu kwenye raundi ya 16 ikiwa Al Ain itashindwa kushinda kwa Manchester City. Kwa upande wake, Manchester City pia inaweza kufuzu kwa raundi ya 16 ikiwa itashinda.
Wydad Casablanca na Al Ain bado hazina alama yoyote na ziko karibu kutolewa nje ya mashindano.
Katika mchezo huo Juventus ilifunga bao la kwanza dakika ya sita kupitia goli la kujifunga la mlinzi wa Wydad, Abdelmounaim Boutouil, baada ya mchezo mzuri wa timu hiyo huku Pasi ya Khephren Thuram ilimpelekea Kenan Yildiz kufumua shuti ambalo lilimgonga Boutouil na kumdanganya golikipa Mehdi Benabid.
Mshambuliaji huyo wa Uturuki, mwenye umri wa miaka 20, aliongeza goli la pili la Juventus dakika ya 16 kwa shuti kali kutoka pembeni ya boksi ambapo Alipokea mpira kwa uhuru, akapiga shuti hilo kwenye kona ya juu kulia, huku Benabid akibaki akishangaa.
Wydad ilipata bao dakika ya 25 baada ya makosa ya ulinzi kutoka kwa Juventus ambapo Nordin Amrabat alitumia pasi fyongo ya Juventus, akampelekea Thembinkosi Lorch mpira kwa usahihi naye akampiga chenga golikipa wa Juventus, Michele Di Gregorio na kufunga.
Goli hilo lilichochea mashabiki wa Morocco, ambao walifukiza vilipukuti vyenye rangi nyekundu na nyeusi, hivyo kusababisha mchezo kusimamishwa kwa dakika kadhaa hadi moshi ukapungua.
Wydad, iliyohitaji angalau sare kuweza kuwa na matumaini ya kufuzu kwenye raundi ya 16 baada ya kufungwa 2-0 na Manchester City katika mchezo wao wa kwanza, ilishambulia kwa nguvu na kuisumbua ngome Juventus.
Hata hivyo, timu ya Italia ilirudisha udhibiti katika nusu ya pili, ikisaidiwa na uingizwaji wa Teun Koopmeiners badala ya Weston McKennie.
Andrea Cambiasso alikaribia kuongeza goli la pili la Juventus dakika ya 55, alipogonga mlingoti kwa volley ya karibu kutoka kwenye kona.
Goli la tatu na la muhimu lilifika dakika ya 69, na Kenan Yildiz akiwa bingwa tena ambapo alipokea pasi nzuri kutoka kwa Randal Kolo Muani, akajikwamua na kumtoka kwa mlinzi mmoja kufunga kwa urahisi sana.
Mchezaji aliyeingia badala, Dusan Vlahovic, alitimiza kalamu ya ushindi wakati wa muda wa nyongeza, akifunga penalti baada ya kufanyiwa faulo na Guilherme Ferreira.
Â