Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameelekeza Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu kuitisha kikao cha dharura kesho Machi 18,2020.
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar-es-salaam majira ya saa 3:00 asubuhi.
Ajenda kubwa kwenye mkutano huo ni kujadili mustakabali wa Ligi Kuu Bara kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambao umeingia nchini mnamo tarehe 15,march 2020 kupitia mwanamama aliyewasili jijini Arusha kupitia uwanja wa KIA akitokea Ubelgiji.