Home Soka Breaking News..Mkude Asaini Simba

Breaking News..Mkude Asaini Simba

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Simba sc Jonas Mkude amesaini kandarasi ya miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo ya kariakoo msimbazi jijini Dar es salaam baada ya mkataba wa awali kumalizika hivi karibuni.

Mkude anayesifika kwa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja amesaini mkataba huo mbele ya Tajiri wa timu hiyo Mohamed Dewji na inasadikwa alisaini kabla ya timu ya taifa kusafiri kwenda katika michuano ya Afcon nchini Misri.

Mkude aliyekulia katika timu ya vijana ya timu hiyo alikua ananyemelewa kwa ukaribu na Yanga ambao walikua tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa ili kumnasa mchezaji huyo ambaye ameachwa na kocha amunike katika kikosi cha taifa stars kilichopo Misri kwa ajili ya michuano mikubwa barani Afrika (Afcon).

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited