Home Soka Simba Sc Yakabidhi Msaada Kateshi

Simba Sc Yakabidhi Msaada Kateshi

by Sports Leo
0 comments

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  leo Desemba 5, 2023 jijini Dar es Salaam amepokea vyakula na bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari, sabuni, unga wa ngano na Maji kutoka kwa uongozi wa klabu ya Simba ikiwa ni msaada kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea Katesh wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Akizungumza mara baada ya kupokea bidhaa hizo Mhe. Ndumbaro ameipongeza klabu ya Simba kwa kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa msaada huo ambao unaenda kusaidia wahanga hao.

Aidha, Mhe. Ndumbaro amevitaka vilabu vingine nchini kuiga mfano huo kwa kutoa msaada kwa jamii ya wana Hanang waliokumbwa na majanga hayo usiku wa kuamkia Desemba 3, 2023 na kusababisha vifo vya watu, kuharibu miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo Barabara pamoja na makazi ya watu wa eneo hilo.

banner

Mhe. Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wa Katesh na watanzania kwa ujumla kwa athari zilizotokea wilayani hanang na kuwatakia matibabu mema majeruhi ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited