Pacome Zouzoua Atwaa Tuzo

Screenshot 20250626 102949 Instagram

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Pacome Zouzoua Atwaa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi juni wa ligi kuu ya Nbc nchini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya ligi kuu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kiungo huyo ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Kibu Dennis sambamba na kiungo Cletous Chama wa klabu hiyo ambao ndio waliingia fainali kwa pamoja.

Kiungo huyo raia wa Ivory Coast aliingoza Yanga sc kushinda michezo mitatu iliyocheza mwezi juni ambapo alifunga mabao matatu na kusaidia upatikanaji wa bao moja ambapo pia alifunga bao katika mchezo wa kuamua ubingwa dhidi ya Simba Sc katika uwanja wa Benjamin Mkapa juni 25 mwaka huu.

Kwa msimu huu hiyo inakua ni mara ya nne kwa kiungo huyo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ambapo pia umekua msimu bora zaidi tangu awasili hapa nchini na wadau wengi wa soka wamemtabiria kuwa anastahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu nchini japo pia atapata ushindani mkali kutoka kwa Jean Charles Ahoua wa Simba sc.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks