Home Soka Lawi Atua Simba sc

Lawi Atua Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka ndani ya Klabu hiyo ni kwamba tayari uongozi wa Simba Sc umemalizana na Beki ya kati kutoka Coastal Union Lameck Lawi baada ya kupeleka kitita cha milioni 205 ambapo Lawi amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Simba kwa makubaliano ya pande mbili.

Beki huyo bora chipukizi wa ligi kuu msimu uliopita amekua na kiwango kizuri kiasi cha kuzivutia klabu kubwa hapa nchini ambapo licha ya kuwa na ofa kutoka timu zingine lakini Simba sc imefanikiwa kumsajili baada ya kukubaliana dau na Coastal Union ambapo alikua na mkataba wa mwaka mmoja umesalia.

Tayari mchezaji huyo ameshasaini mkataba huo na sasa anachosubiri ni utambulisho pekee hasa pindi ligi kuu itakapomalizika na dirisha la usajili kufunguliwa.

banner

Lawi ambaye ni mrefu anakuja wakati muafaka ambapo mabeki wa kati ya Simba sc Hussein Kazi na Kennedy Juma wamekua na mwenendo wa kusuasua hasa anapokosekana Henock Inonga ambaye dalili zinaonyesha anaweza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited